preety boy

preety boy
ya boy

Wednesday, December 8, 2010

KUWA MAKINI NA UTUMIAJI WA FACEBOOK.


Ni takribani mwaka mmoja na nusu sasa tangu nimejiunga na huu mtandao wa kuwasiliana na marafiki.( facebook)..sio siri nimepata marafiki wengi sana ambao nilikuwa sijuani nao kabla, unapoishi na watu tegemea mazuri na mabaya na sio wote watakao kupenda,hivi ndivyo ilivyo na ndivyo ilivyonitokea katika matumizi ya facebook,nimepata marafiki wengi lakini kati ya hao walikuwepo walioonesha kuwa pamoja nami na wale ambao nilienda nao tofauti,sijafahamu ni kwanini tuliendana tofauti lakini ukweli i kwamba ilitokea mikwaruzo ya hapa na pale, Facebook ina matumizi mazuri na mabaya na ni sisi wenyewe watumiaji ndio tunayoitumia vibaya kwa kupeana status zenye majungu ,kuchukiana na kusemana na hata kutumiana sms za mapenzi bila idhini yako,mtu kukuharasi na hata kutumiwa comments au sms zenye lugha chafu. Sikupenda baadhi ya mambo niliyokutana nayo,nilifanya mistakes lakini niliwaomba msamaha wale wote ambao niliwafanyia vibaya.nimejitahidi kuwapenda marafiki zangu wote na naendelea kufanya hivyo ingawa kuna baadhi ya marafiki hawapendeki.
Facebook ina mambo mengi sana mazuri na mabaya hivyo tujaribu kuitumia
vizuri.

................................................................preety hans.........................................................................